Chati ya muziki duniani ya Billboard Hot 100 chart imethibitisha kuwa wimbo wa rapa Wiz Khalifa Ft Charlie Puth “See You Again ” Umeweka rekodi ya kuwa miongoni mwa nyimbo zilizoshika namba moja na kuka kwenye nafasi hio kwa muda mrefu zaidi.
Wimbo huu uliotumika kwenye filamu kubwa ya Furious 7 imeshika rekodi sawa na nyimbo hizi mbili ambazo ni Black Eyed Peas “Boom Boom Pow” na ya Eminem “Lose Yourself.”
Wiz Khalifa amefikia rekodi hiyo kwa wimbo wake kukaa kwenye nafasi ya kwanza kwa wiki 13 mfululizo bila kushuka.
Rekodi nyingine ni kuwa hawa ndio rapa walio na nyimbo zilizokaa namba moja kwa muda mrefu zaida kwenye bilboard Wiz Khalifa, Eminem, Black Eyed Peas, Puff Daddy, Flo Rida, Kanye West, na Nelly
0 comments:
Post a Comment