Msimu wa 15 wa kipindi cha kutafuta vipaji cha “American Idol” kimetangazwa kuwa ndio msimu wa mwisho wa kipindi hichi kitakachoanza kuonyeshwa January 2016.
Msimu wa 15 utasimamiwa na Mtangazaji Ryan Seacrest akiwa na majaji Jennifer Lopez, Keith Urban na Harry Connick Jr.
Wasanii waliopata mafanikio kutoka kwenye show hii ni pamoja na Fantasia Barrino, Jennifer Hudson, Jordin Sparks, Kelly Clarkson na Carrie Underwood. Inasemekana sababu ya kufuta show hii ni upungufu wa utazamaji wa watu, Show imekuwa ikitazamwa na watu zaidi ya milioni 30 ila mwaka jana 2014 ilitazamwa na watu milioni 10.6.
0 comments:
Post a Comment