Christian Ronaldo ni moja ya wachezaji ambao wanatengeneza pesa nyingi sana kwa mwaka, Ronaldo anaamini kuwa bila wakala wake Jorge Mendes hangeweza kupata mafanikio makubwa kama aliyonayo sasa.
Ronaldo anampenda sana wakala wake, na sio kwamba alikuwa bestman wake kwenye harusi tu, Ronaldo pia amempatia zawadi moja kubwa sana wakala wake huyu.
Ronaldo amempa zawadi ya kisiwa kizima katika nchi ya Ugiriki, Ugiriki imeanza kuuza visiwa kutokana na hali mbaya ya uchumi inayoikabili nchi hiyo, kisiwa kimoja kinauzwa katika ya dola million 3.28 mpaka dola million 54.8.
0 comments:
Post a Comment