TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA ILI UPATE MAFANIKIO KWA HARAKA ZAIDI

TANGAZA BIASHARA YAKO HAPA ILI UPATE MAFANIKIO KWA HARAKA ZAIDI
Home » » Hii ni mpya kuhusu usajili Kipa wa Man United David De Gea.

Hii ni mpya kuhusu usajili Kipa wa Man United David De Gea.

Moja kati ya Story ambazo zimeteka hisia za mashabiki wengi wa soka bila kusahau vyombo vya habari za michezo bila shaka ni story ya usajili wa kipa Muhispania David DeGea ambaye ulimwengu mzima unafahamu kinachoendelea kati yake na klabu mbili za Real Madrid na Manchester United.Jarida moja la kila siku Hispania limeripoti kuwa kipa huyu atakuwa mchezaji wa Real Madrid mpaka ifikapo jumamosi ya wiki hii wakati ambapo Ligi Kuu ya England itakapokuwa ikianza rasmi msimu wake wa2015/2016.
david_de_gea-465786
Taarifa hii inazidi kupata nguvu kutokana na tetesi ambazo zilizuka hapo jana ambapo kocha wa United,Louis Van Gaalaliripotiwa kusema kuwa angependa kuona DeGea akiuzwa kutokana na hali inayoendelea kuleta sintofahamu ndani ya timu.Madrid watamsajili De Gea mpaka kufikia jumamosi ya wiki hii.Real Madrid imepanga kumfanya De Gea kuwa kipa wake namba moja baada ya kuondoka kwa Iker Casillas ambaye ameitumikiaMadridkwa muda wa miaka 25 karibu miaka 18 kati ya hiyo akiwa kipa namba moja.Endapo United itakubali kumuuza De Gea katika wakati huu huenda wakajikuta kwenye wakati mgumu kutokana na kutokuwa na mtu ambaye timu hii imemuandaa kuwa mrithi wa De Gea huku wakiwa hawajaanza mazungumzo na kipa yoyote yule.Kulikuwa na stori kwamba United imekuwa ikiigomea Madrid kuhusu De Gea huku wakisema wanahitaji kulipwa pound milioni 40 kwa ajili ya kipa huyo na Madrid wakiwa tayari kulipa pound milioni 25 pekee.
Share this video :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Creating Website | WILLE Template | GOOGLE
Copyright © 2013. Dj Wille Zedon - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Mas Template
Proudly powered by Blogger